Miaka kadhaa baada ya Gardner G. Habash kujivua u-Captain wa kipindi cha Jahazi cha Clouds Fm na kuving’arisha vipindi vya jioni vya radio pinzani kwa kituo hicho, mtangazaji huyo mahiri amesaini mkataba wa kurejea katika kituo hicho.

Gardner anarejea Clouds Fm ikiwa ni miaka kadhaa tangu alipoanchana na radio hiyo iliyoingia kwenye beef kubwa la kibiashara na mkewe wa zamani, Lady Jay Dee.

Baada ya kuondoka Clouds Fm, Gardner alijiunga na Times Fm na kuongoza kipindi cha jioni cha ‘Maskani’ kabla ya kuhamia E-FM kuongoza kipindi kingine cha jioni kinachojulikana kama ‘Ubaoni’.

Katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la kuhama kwa watangazaji mahiri wa vituo vya redio shindani jijini Dar es Salaam. Hivi karibuni, waliokuwa watangazaji wa Power Break Fast ya Clouds Fm, Paul James (PJ) na Gerald Hando walihamia E-Fm huku taarifa za awali zikieleza kuwa Masoud Kipanya na Fina Mango wamerejea kwenye kipindi hicho baada ya kuondoka miaka kadhaa iliyopita.

Baadhi ya watangazaji na Ma-DJ wa Times Fm nao wameelekea E-FM, akiwemo aliyekuwa mtangazaji mahiri wa kipindi cha The Jump Off, Jabir Salehe ambaye sasa anatangaza ‘Ladha 3600’ katika kituo chake kipya (E-FM).

Serikali yakanusha kunyimwa misaada na nchi za Magharibi
Ander Herrera: Tutamaliza Ligi Juu Ya Man City