Kocha wa muda wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate huenda akathibitishwa kuwa kocha mkuu juma lijalo, kufuatia mazungumzo aliyoyafanya dhidi ya viongozi wa cha cha soka cha nchi hiyo FA.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports, Southgate alifanyiwa usahili na timu ya watu watano kutoka FA hapo jana, na kwa kiasi kikubwa ameonyesha kuimudu kazi aliyoifanya kwa muda.

Mtendaji mkuu wa FA Martin Glenn, alikiambia kituo cha televisheni cha Sports News kwamba, Southgate yupo katika nafasi nzuri ya kuajiriwa kutokana na utendaji wake wa kazi kuridhisha.

Hata hivyo Glenn hakuzungumzia suala la usahili kwa kocha huyo ambapo alisema ilikua ni mapema kulizungumza hilo katika vyombo vya habari, lakini uchunguzi uliofanywa na kituo hicho cha televisheni umebaini jana taratibu hizo zilifanyika.

Katika timu ya watu watano wa FA waliomfanyia usahili Southgate, Glenn alikua miongoni mwao sambamba na mwenyekiti wa Greg Clarke, mkurugenzi wa ufundi Dan Ashworth, Graeme Le Saux pamoja na Howard Wilkinson.

Viongozi wa dini wamtaka Makonda kumuomba radhi Kamanda Sirro
Ridhiwani aeleza kwanini hufanya ibada ya Mizimu