Kocha wa muda wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate, amesema atalazimika kumpima utimamu wa mwili mshambuliaji wa Spurs Harry Kane, kabla ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Scotland ambao utachezwa mwishoni mwa juma hili.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ametajwa katika kikosi cha England ambacho kinaingia kambini hii leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Scotland, baada ya kuwa nje kwa muda wa majuma saba kufuatia majeraha ya goti yaliyokua yakimsumbua.

Hata hivyo kurejea kwake uwanjani kumeipa faraja Spurs katika mchezo wa jana dhidi ya Arsenal, kutokana na juhudi zake za kufunga bao la kusawazisha kwa njia ya mkwaju wa penati.

Kane hakuwa sehemu ya kikosi cha England ambacho mwezi uliopita kilicheza michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Malta na Slovenia, kufuatia majeraha yaliyomkabili kwa muda mrefu.

“Nitamfanyia majaribio ya mwili ili kujua utimamu wake kwanza, halafu mambo mengine yatafuata ili kufahamu kama ataweza kuwa sehemu ya kikosi katika mchezo dhidi ya Scotland siku ya ijumaa.” Amemsea Southgate.

George Lwandamina Abwaga Manyanga Zesco United
Lukaku: Paul Pogba Anastahili Ballon d'Or 2016