Gari lililokuwa kwenye msafara wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limegongana na gari la moja la Zambia jijini Lusaka, jana asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya Mwebantu, dereva wa gari hilo la Zambia aliyetajwa kwa jina la Andrew Phiri alifariki katika ajali hiyo ambapo magari hayo yaligongana uso kwa uso.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la barabara ya Leopards Hill, mukabala na balozi za Saudi Arabia na Ufaransa.

Rais Kabila alikuwa nchini Zambia kwa ziara maalum. Dereva wa gari hilo la msafara wa Kabila alikimbia na imeelezwa kuwa hakupata majeraha makubwa.

Mwili wa Akwilina wafanyiwa uchunguzi Muhimbili
Video: Linah aja na ''Same boy'' kama ya R-Kelly na Usher ''same girl''