Gari la mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, jana lilimgonga na kusababisha kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka 14, katika eneo la Iyunga, barabara kuu ya Mbeya – Tunduma.

Dereva wa Mbunge huyo aliyetajwa kwa jina la Gabriel Andrew, aliyekuwa anaendesha gari hilo lililomgonga mtoto Rachel Lutumo katika eneo la wavuka kwa miguu anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kufikishwa mahakamani.

Taarifa kutoka mkoani Mbeya zimeeleza kuwa, ajali hiyo ilitokea wakati mbunge huyo akielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kuwapokea viongozi wa kitaifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari Mtoto huyo alifariki dunia alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya, kwa kutumia gari hilo lilomgonga aina ya Toyota Land cruiser.

Mtoto huyo ametajwa kuwa yatima aliyekuwa akiishi na bibi yake na kwamba alikuwa amemaliza elimu ya msingi na kufaulu kujiunga na kidato cha kwanza. Hivyo, alitarajia kuanza elimu ya sekondari mwezi ujao.

Serikali kuwasha umeme vijiji vyote nchini mwakani
Maalim Seif afunguka kuhusu Lipumba ‘kumshawishi’ Lowassa, amsifu Rais Magufuli