Watu 14 wamekufa na wengine 22 kujeruhiwa baada ya gari lililosheheni mabomu kulipuliwa karibu na hoteli moja jijini Mogadishu nchini Somalia.

Maafisa wa vyombo vya usalama wamesema kuwa tukio hilo la kigaidi lililotokea jana lilifuatiwa na mashambulizi ya risasi.

mashuhuda wa tukio hilo wameliambia shirika la habari la AFP kuwa waliona gari hilo likisogea karibu na hoteli hiyo kwenye mtaa ambao una watu wengi na muda wa msongamano wa magari. Barabara hilo hutumiwa zaidi na maafisa wa Serikali na huwa na ulinzi mkali.

Video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha gari la hospitali likifika katika eneo hilo na kuwachukua majeruhi baada ya mlipuko.

Kundi la kigaidi la Al Shabaab limedai kuhusika na tukio hilo. Kundi hilo lenye ushirikiano na Al Qaeda linafanya mashambulizi ya kigaidi likilenga kuiondoa madarakani Serikali inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi.

Jeshi la Polisi lafanya oparesheni kali, laibua mazito
Sarkozy alia na rushwa ya Gaddafi, ‘naishi kama kuzimu’