Gari lililotumika kumteka mfanyabiashara, Mohamed Dewji na dereva aliyekuwa akiendesha limejulikana kuwa ni aina ya Surf.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ambapo amesema kuwa kupitia vyombo vya uchunguzi vilifanikiwa kukamata ganda la risasi yenye urefu wa milimita 9 ambazo ilitumika wakati wa tukio la kupotea kwa Mohamed Dewji.

Amesema gari hilo limesajiliwa kwa namba za usajili za kutoka nchi jirani ambapo inaelezwa gari hilo lilifanikiwa kuingia mwanzoni mwa mwezi septemba mwaka huu.

“CCTV Camera zimetusaidia zimeweza kutambua gari baada ya kufanya uchunguzi tumefanikiwa kulijua gari na tumezungukia maeneo yote ambayo hilo gari lilipita na bado watu wetu wameendelea kufuatilia kama gari lilielekea maeneo ya Silver sand au Kawe.” amesema Kamanda Sirro

Aidha, amesema kuwa wamepata taarifa kwamba gari hilo limetokea nchi jirani, na maafisa usalama wamekwenda mpakani na wameona gari hilo lilipita mpakani tarehe moja septemba, na kumfahamu dereva wa gari lile, huku bado  interpool wanalifanyia kazi.

Hata hivyo, IGP Sirro amewataka watu wenye uwezo wa kifedha nchini kujiwekea ulinzi wa kutosha kwa ajili ya usalama wa maisha yao.

Hatua 5 za Kuchukua Mfanyakazi Mwenza Akijisifia Kwa Kazi Yako
LIVE IKULU: Rais Magufuli akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars)