Meneja wa klabu ya Middlesbrough Garry Monk, ameendelea kusisitiza suala la kutomuweka sokoni Ben Gibson katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Gibson amekua gumzo la muda mrefu, kufuatia klabu za Southampton na West Brom zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini England (PL), kujitokeza hadharani na kueleza namna wanavyojipanga kumsajili beki huyo.

Boro kupitia kwa meneja wao Monk, amekua wakipuuza taarifa hizo mara kwa mara, lakini bado viongozi wa Southampton na West Brom wanaendelea kuamini usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 24, utawezekana kabla ya dirisha halijafungwa mwishoni mwa mwezi huu.

“Ninahitaji kuwa na kikosi imara ambacho kinaundwa na wachezaji wenye umuhimu mkubwa, hata mwenyekiti wa klabu (Steve Gibson) analijua hilo,” alisema Monk.

“Hatutomuuza mchezaji yoyote katika kipindi hiki, japo ninaendelea kusikia na kuona kupitia vyombo vya habari kuhusu baadhi ya wachezaji wangu wakizungumzwa kuwa katika soko la usajili katika kipindi hiki ambacho mambo mengi hujitokeza.

“Tunahitaji kufanya kazi na hatuzipi nafasi taarifa hizo, kwa sababu tunajua kama tutafanya hivyo tutapoteza muda wa kufanya maandalizi mazuri ya kujiandaa na mtihani wa mapambano yaliyo mbele yetu.”

Ben Gibson ni mpwa wa mwenyejiti wa klabu ya Middlesbrough  Steve na Monk ambaye ni mkuu wa benchi la ufundi, baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo mwezi Juni mwaka huu.

Inter MIlan Yasajili Beki Wa Kibrazil
Liverpool FC Yaikatalia FC Barcelona