Uongozi wa klabu ya SSC Napoli unakaribia kumsainisha mkataba mpya meneja wa klabu hiyo Gennaro Ivan Gattuso, baada ya kuridhishwa na kazi yake tangu alipoajiriwa mwishoni mwa mwaka 2019.

Taarifa zilizothibitishwa na mkurugenzi wa SSC Napoli Cristiano Giuntol zimeeleza kuwa Gattuso mwenye umri wa miaka 42, ameonesha kuwa tayari kusaini mkataba mpya na wakati wowote watakamilisha mpango huo.

Giuntoli ameweka hadharani jambo hilo alipohojiwa na kituo cha Televisheni cha Sky Sport Italia, baada ya SSC Napoli kuambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja kwenye michuano ya Europa League dhidi ya AZ Alkamar ya Uholanzi.

“Najua mawakili wanabadilishana mikataba,” Giuntoli aliiambia Sky Sport Italia.

“Tumefikia makubaliano na makaratasi yameandikwa juma hili. Sidhani kama kutakuwa na shida.”

“Gattuso anasumbuliwa zaidi kila siku kuliko Carlo Ancelotti, lakini hiyo ni tabia yao tu. Wote ni wataalamu wazuri.”

Gattuso amekua na matokeo ya kuridhisha tangu alipokabidhiwa kikosi cha SSC Napoli, akichukua nafasi ya Carlo Ancelotti mwezi Desemba 2019, huku akishinda ubingwa wa Coppa Italia msimu 2019-20, likiwa taji la kwanza la klabu hiyo tangu mwaka 2014.

Afariki mara mbili
Njaa yapelekea raia kula mchanga- Madagascar