Naibu Gavana wa jimbo la Ikweta Kusini Magharibu mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ,Tathy Bikamba ameshtakiwa kwa tuhuma za ubakaji wa binti wa miaka 20 ambaye inadaiwa kuwa alimfanyia unyama huo baada ya kumpa dawa za kulevya.

Gavana huyo anatarajiwa kufikishwa Kinshasa kujibu tuhuma hizo mahakamani , ingawa wakili wake amezipuuza tuhuma hizo.

Taarifa kutoka za uchunguzi wa kesi hiyo ya ubakaji zinasema kuwa gavana huyo alimbaka binti huyo siku ya Jumamosi.

Aidha, Bikamba ambaye kwa sasa yuko gerezani anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo ili aweze kujibu mashtaka yake ya kumwekea dawa ya kulevywa na kumfanyia tendo la ngono binti bila ridhaa yake.

Hata hivyo, Waziri wa sheria wa nchi hiyo,Faida mwangiliwa ambaye pia ni miongoni mwa wanaharati wa haki za wanawake ameomba sheria kumshughulikia vikali gavana huyo ikiwa tuhuma hizo zitathibitishwa na mahakama.

 

Marekani yalalama baada ya China kulipiza kisasi
Museveni azungumza na Askofu Mkuu kuhusu tuhuma za 'kumpindua'

Comments

comments