Bunge la Seneti nchini Kenya limepiga kura kumuondoa Mike Mubuvi Sonko, kama gavana wa Nairobi,   hatua ambayo imekomesha miaka mitatu ya utawala wake uliogubikwa na utata.

Sonko anatuhumiwa kwa ukiukaji wa katiba, matumizi mabaya wa mamlaka, utovu wa nidhamu, na uhalifu chini ya sheria.

Maseneta 27 walipiga kura kuunga mkono kuondolewa ofisini kwa Sonko kwa kudumisha mashtaka yote manne yaliyowasilishwa na Bunge la Kaunti ya Nairobi, ambalo lilipiga kura ya kutokuwa na imani naye mnamo Desemba 3.

Kuondolewa madarakani kwa Sonko kumetoa nafasi kwa Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Ben Mutura, kushikilia wadhifa huo hadi uchaguzi wa Gavana na Naibu wake utakapofanywa katika kipindi cha siku 60 zijazo.

Ligi Kuu: Msako wa alama tatu kuendelea
Simba SC yaifuata FC Platnum