Gavana wa Kundi laTaliban kutoka jimbo la Panjshir Mawlawi Qudratullah anusurika katika shambulizi la bomu katika mjini Kabul. 

Naibu mkuu wa polisi wa Panjshir Abdul Hameed Khurasani, amesema bomu lililotegwa kando ya barabara lililipuka wakati msafara wa Gavana huyo ukipita katika eneo la Taimani. 

Hata hivyo Khurasani amesema kwamba hakuna aliyedhurika na mlipuko huo. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Qari Saeed Khosty amethibitisha kutokea kwa mlipuko huo lakini hakutoa maelezo zaidi. 

Video zilizochapishwa kwenye miitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mwingi katika eneo hilo na cheche za moto kutoka kwa njia za umeme. Hakukuwa na madai ya mara moja ya kuhusika na shambulio hilo lakini kundi linalojiita Dola la Kiislam limejinasibu kwa mashambulizi kama hayo.

Rais Samia amtembelea Mama Maria Nyerere
Kura zaendelea kuhesabiwa Nchini Gambia matokeo ni haya