Wapinzani wa Young Africans katika mchezo wa kwanza ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Sagrada Esperanca ya Angola wamewasilia usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo huo ambao utachezwa kesho katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Angola imefikia katika hoteli ya Protea na jioni ya leo itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka, Joseph Odartei Lamptey atakayepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera David Laryea na Malik Alidu Salifu, wakati Kamisaa ni Asfaw Luleseged Begashaw kutoka Ethiopia.

Mchezo wa marudiano utachezeshwa na waamuzi wa Madagascar Mei 17, mwaka huu Uwanja wa Sagrada Esperanca, zamani Quintalao do Dundo.

Waamuzi hao ni Hamada el Moussa Nampiandraza atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean Thierry Djaonirina.

Young Africans imeangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.

Young Africans ilianza vizuri kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.

Kwa upande wao, Sagrada Esperanca katika Raundi ya Awali waliitoa Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1 ugenini na kushinda 2-0 nyumbani.

Katika Raundi ya kwanza wakaitoa LD Maputo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda 1-0 nyumbani na kutoa sare ya 1-1 ugenini na kwenda hatua ya 16 Bora, ambako waliitoa V. Club Mokanda ya Kongo kwa jumla ya mabao 4-1 wakishinda 2-1 ugenini na 2-0 nyumbani.

Jamuhuri Kiwelu Julio Awabwatukia Viongozi Wa Simba
Joseph Odartei Kuchezesha Game Ya Young Africans Vs Sagrada Esperanca