Shirikisho la soka nchini Ethiopia (EFF) limemteua Gebermedhin Haile kukaimu nafasi ukocha wa timu ya taifa kwa muda.

Kamati ya Utendaji ya EFF imeamua kumteua Haile, ambaye anafundisha timu ya Jeshi la nchi hiyo kuwa kocha wa Walias kwa makubaliano ya muda mfupi.

“Shirikisho limesaini Mkataba wa muda mfupi na kocha Gebremedhin Haile. Mkataba huo utaanza Mei 9, 2016 hadi Oktoba 9, mwaka 2016,” taarifa ya EFF imesema.

 Kocha Gebermedhin Haile

Haile anakabiliwa na jukumu la kushinda mechi mbili zilizobaki za kufuzu AFCON mwaka 2017. Ethiopia itasafiri hadi Maseru kucheza na Lesotho mwezi Juni kabla ya kuhitimisha kampeni zake kwa kumenyana na Shelishelei Septemba.

Haile anachukua nafasi ya Yohannes Sahle ambaye Mkataba wake ulivunjwa wiki chache zilizopita kutokana na matokeo mabaya.

Yohannes Sahle ambaye Mkataba wake ulivunjwa wiki chache zilizopita kutokana na matokeo mabaya.

Haile, mshambuliaji hatari enzi zake anacheza timu ya taifa ya Ethiopia na aliyewahi amefundisha timu za nyumbani kwao kwa mafanikio zikiwemo Trans Ethiopia, Ethiopian Insurance, Ethiopian Coffee na Dedebit.

Alikuwa kocha Msaidizi wakati Ethiopia inatwaa ubingwa wa CECAFA Challenge mwaka 2004, na tayari ameiwezesha Defence Force kutwaa mataji mawili ya Kombe la Ethiopian.

Jukumu lake la kwanza litakuwa ni mchezo wa kufuzu AFCON 2017 dhidi ya Lesotho Juni.

Kinnah Phiri Atoa Sababu Za Kufungwa Na Young Africans
Kamati Ya Marekebisho Katiba Ya ZFA Yahitaji Mamilioni Ya Shilingi