Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Klabu ya Geita Gold FC Hemed Kivuyo amesema, Uongozi wa Klabu hiyo unajua cha kufanya wakati wa Dirisha Dago la Usajili, ambalo litafunguliwa Rasmi Desemba 16 ma kufungwa Januari 15-2023.

Geita Gold FC imeshatangaza kufanya usajili wa baadhi ya wachezaji kupitia Dirisha Dogo, kufuatia mapungufu yaliyojitokeza kwenye kikosi chao, baada ya kucheza michezo 15 ya Mzunguuko wa Kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kivuyo amesema Uongozi umejipanga kufanya usajili kwa utulivu ili kuepuka Mihemko, ambayo inaweza kuwaletea changamoto ya kupata wachezaji, ambao huenda wakashindwa kuisaidia Timu katika Michezo 15 iliyosalia hadi mwishoni mwa msimu huu.

“Hatutasajili kwa Mihemko kwa sababu tunajua hapa ndipo tunatakiwa kufanya usajili kwa kutulia, Wachezjai watakaosajiliwa watatakiwa kuongeza kitu kwenye kikosi chetu, ikitoea wanashindwa ni sawa na bure.”

“Kwa mujibu wa Ripoti ya Kocha wetu ni dhahir tutasajili, kwa hiyo Mashabiki wetu wanapaswa kuendelea kuwa watulivu na kuona tutamsajili nani wakati wa Dirisha Dogo, ili kufikia malengo tuliojiwekea kwa msimu huu.”amesema Kivuyo

Geita Gold FC inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa Msimu wa Pili mfulilizo, na hadi sasa imeshajikusanyia alama 22 zinazoiweka katika nafasi ya Tano katika Msimamo.

Makamba, Bi. Koch wajadili ujenzi mradi wa gesi asilia
Mtibwa Sugar yasubiri ripoti ya Mayanga