Uongozi wa Geita Gold FC umethibitisha kuachana rasmi na Mshambuliaji George Mpole, baada ya Mkataba wa Pande hizo mbili kufikia kikomo leo Jumanne (Desemba 07).

Mpole alibuka Mfungaji Bora Msimu wa 2021/22, akifunga mabao 17, mbele ya Mshambuliaji hatari wa Young Africans Fiston Mayele aliyefunga mabao 16.

Geita Gold FC imethibitisha kuachana na Mshambuliaji huyo, kwa kuandika Barua maalum ya kumfahamisha Mpole kuhusu Mkataba wake kufikia kikomo.

Kwa juhudi zetu Dar24 Media tumefanikiwa kuinasa barua ya Geita Gold FC ambayo imeandikwa na kuwasilishwa kwa Mshambuliaji Mpole.

Wengine wanaswa sakata la dawa za kulevya
DCEA yawashikilia saba kwa kukutwa na Dawa za kulevya