Uongozi wa Geita Gold FC umeweka wazi mikakati waliyoyano ya kuhakikisha kikosi chao kinarejea katika Michuano ya Kimataifa msimu ujao wa 2023/24 na kuwa bora Zaidi ndani nan je ya Uwanja.

Geita Gold FC kwa mara ya kwanza ilishiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23, na kuondolewa katika hatua ya awali kwa faida ya bao la ugenini dhidi ya Hilal Alsahil ya Sudan, ikipoteza ugenini 1-0 na kupata ushindi wa 2-1 nyumbani Tanzania.

Katibu Mtendaji wa Geita, Simon Shija amesema wamedhamiria kuona wakirejea katika Michuano hiyo ya Kimataifa, baada ya kujifunza mambo mengi kutoka katika klabu za Simba SC na Young Africans, ambayo wanaamini yatawasaidia endapo watapata nafasi.

Amesema wanaamini kufanya vizuri kwa klabu za Simba SC na Young Africans katika Michuano ya Kimataifa kumetokana na uzoefu wa muda mrefu na uwekezaji mkubwa uliowekwa ndani ya klabu hizo.

“Tumejipanga kuhakikisha tunamaliza katika nafasi nne za juu ili tuwe sehemu ya timu zitakazowakilisha nchi kimataifa msimu ujao, kama tutafanikisha hili, itakuwa ni mara yetu ya pili mfululizo.”

“Kuna mambo mengi tumejifunza na kutambua wapi tulipokosea mwanzoni mwa msimu huu tuliposhiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho, tunaamini tukirudi tena tutakuwa imara zaidi.”

“Klabu za Simba SC na Young Africans zinasajili, kulipa mishahara mizuri kwa wakati, bonasi na kuweka kambi sehemu yoyote, hivyo inaleta motivation kwa wachezaji kufanya vizuri, kwetu klabu ndogo hili linatupa hamasa kubwa,”

“Nasi tunatamani kupata udhamini kama huo tuweze kuwahudumia vizuri wachezaji wetu na tufike huko, Geita Gold tuna mikakati mizito kuhakikisha tunarudi kimataifa msimu ujao tukimaliza kwenye nafasi nne za juu, nia tunayo wadhamini wetu wapo tayari na mazungumzo mbalimbali yanaendelea.”

“Sisi kama timu tutapambana tusitoke kwenye nafasi tuliyopo, pili kupambana kwa nguvu zote kupigania nafasi nne za juu japokuwa waliopo juu yetu wanatuzidi alama nyingi.” Amesema Simon Shija

Geita Gold kwa sasa inahaha kuingia Nne Bora ya Ligi Kuu hadi sasa ikiwa imekusanya alama 34 ikishika nafasi ya tano nyuma ya Azam FC na Singida Big Stars zilizopo juu yao nafasi ya tatu na ya nne.

Dkt. Mwinyi: Zanzibar imefungua milango ya uwekezaji
Wachezaji Taifa Stars wala kiapo Misri