Katika kutekeleza wito wa Mh. Rais John Pombe Magufuli wa kuchangia sekta ya Elimu ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira bora  Mgodi wa madini ya dhahabu Geita (Ggm) umechangia jumla ya milion 44 sawa na madawati 6000 siku chache zilizopita.

Akizungumza katika harambee za uchangiaji wa madawati uliofanyika siku chache zilizopita Mkoani  Geita  Mkurugenzi mtendaji wa Ggm Bw. Terry Mulpeter  Alisema kuwa elimu  ni chachu ya ukombozi wa Taifa hivyo Mgodi huo utaendelea kuunga jitihada za serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

Aidha Bw. Mulpeter aliongeza kuwa mazingira mazuri ya kusomea humpa mwanafunzi fursa ya kufanya vizuri katika elimu ya msingi mpaka kufikia ngazi za juu huku akisisitiza kwamba elimu ni haki muhimu kwa watoto na kwamba huwasaidia kujikomboa kiuchumi na fikra.

 Mulpeter alimhakikishia Naibu waziri ofisi ya Rais (Tamisemi) Seleman Jafo kuwa Mgodi wake upo kwa ajili ya kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa elimu bora inapatikana na kwamba Ggm imeboresha mazingira ya wanafunzi zaidi ya 800 katika shule ya wasichana Nyankumbu Geita kusoma kwa vitendo huku walimu wakijengewa nyumba bora za kuishi lengo likiwa ni kuboresha elimu ndani ya mkoa huo.

Pamoja na hayo Mkoa huo umekusanya pesa taslimu bilion 1.7 Kutoka kwa wadau mbalimbali wapenda maendeleo ambapo fedha hizo zinakadiriwa kununua madawati yasiyopungua 23000 , na kufanya kiwango hicho kupunguza uhaba wa madawati kwa asilimia 34 ya upungufu uliopo sasa.

Video: Makonda ashiriki usafi na JWTZ, Atangaza Oktoba 1 siku ya kupanda miti
Cheyo Huyu Ndiye Raisi Tunaemhitaji