Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,John Magufuli ,ambae anasaka nafasi ya kuchangulia katika  uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Amehaidi kujenga barabara ya kutoka Geita hadi kahama kwa kiwango cha lami.

Akihutubia wanachama wa CCM na wananchi wilani Chato  mkoa Geita ,amesema kuwa atasimamia ilani ya chama hicho kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo itakayoboresha utalii katika eneo la kanda ya ziwa .

“Barabara ya Geita, Bukori hadi Kahama tutaijenga kwa lami mara tu mtakapomaliza kutuchagua. Na haya tumeyafafanua vizuri kwenye kitabu cha ilani ya uchaguzi ya CCM,” amesema Magufuli.

Magufuli amesema kuwa serikali ya CCM  inajenga uwanja mkubwa  wa ndege pamoja na daranja la  Busisi  mkoani Mwanza ili kuongeza na kukuza soko la utalii.

“Tunajenga uwanja mkubwa pale Mwanza, watalii wawe wanatoka Ulaya wanateremka Mwanza wakishatoka wasihangaike kupanda Kivuko na watapita kwenye daraja la Kilomita 3.2 pale Kigongo BusisI ambalo nalo ni utalii tosha”amesema Magufuli.

Bofya hapa …

Kagere bado yupo yupo sana Msimbazi
Sumaye: Wapuuzieni wanaowasema vibaya wagombea