Ombi la kiungo wa klabu ya Valencia ya Hispania, Geoffrey Kondogbia la kuitumikia timu ya taifa ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati, limekubaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, aliomba uthibitisho kutoka FIFA wa kutaka kutambuliwa kama raia wa Jamuhiri ya Afrika ya Kati, akitokea Ufaransa ambapo ndipo alikua anatambuliwa kisoka, baada ya kulitumikia taifa hilo la barani Ulaya katika fainali za kombe la dunia chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2013.

Kondogbia amekuwa mchezaji mwenye bahati ya kukubaliwa na FIFA kucheza katika mataifa mawili kwa upande wa timu za wakubwa, kwani aliwahi kutumika kama mchezaji wa akiba katika kikosi cha Ufaransa wakati kikiwa kwenye harakati za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia 2014 dhidi ya Belarus Septemba 2013.

Pia, wasifu wake unaonyesha amewahi kucheza mara tano katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Hata hivyo, Kondogbia atalazimika kusibiri wakati mwingine, kuanza kuitumikia jamuhuri Ya Afrika ya Kati, kutokana na mejraha yanayomkabili kwa sasa.

Tayari kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamuhuri Ya Afrika ya kati Raoul Savoy alikua ameshamjumisha kwenye kikosi chake, ambacho mwishoni mwa juma hili kitakabiliwa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika 2019 dhidi ya Guinea.

Kiungo Quentin Ngakoutou ameitwa na kocha huyo kuziba nafasi ya Kondogbia, huku matarajio makubwa ya kiungo huyo kuanza kuonekana akiw ana jezi ya taifa hilo la Afrika, yatakua kwenye mchezo dhidi ya Ivory Coast mwezi Oktoba.

Ndugu wa kiungo huyo aitwae Evans tayari ameshaitumikia timu Jamuhuri Ya Afrika ya kati katika michezo mitano.

Savoy ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa aliwahi kufanya maamuzi ya kurejea katika taifa la asili ya wazazi wake, na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Guinea mwishoni mwa juma hili.

Kondogbia alianza kucheza soka katika ngazi ya klabu akiwa na Lens Ufaransa, kabla hajatimkia nchini Hispania kujiunga na Sevilla CF Julai 2012, baadae alirejea Ufaransa kujiunga na AS Monaco (2013–2015), Inter Milan (2015–2018) na sasa yupo Valencia tangu Agosti 2017.

Image result for Frederic NimaniFrederic Nimani

Wakati huo huo FIFA imemruhusu Frederic Nimani wa klabu ya Xamax ya Uswiz kuitumikia Jamuhiri Ya Afrika ya kati katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Guinea. Niami ni mzaliwa wa Ufaransa na amewahi kucheza katika kikosi cha vijana cha nchi hiyo.

Jamuhiri ya Afrika ya kati ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi H, baada ya kuifunga Rwanda mabao mawili kwa moja katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza mwezi Juni 2017. Guinea wanaongoza msimamo wa kundi hilo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, baada ya kuibanjua Ivory Coast mabao matatu kwa mawili.

Video: Ni lazima King'anya akamatwe- JPM
Serikali kuongeza fedha za TASAF