Patashika za michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika zimeanza rasmi mwezi huu, wakati Yanga ya Tanzania ikisafiri kuwafuata wapinzani wao Sekho De Joackim ya Mauritius, nchini Uganda kutakuwa na pambano la kukata na shoka pale ambapo Vipers FC itakapo waalika Enyimba FC ya nchini Nigeria.

Kocha mkuu wa Vipers FC, George ‘Best’ Nsimbe amesema anawajua vizuri Enyimba na yupo tayari kwa pambano lao litakalopigwa Uwanja wa Nakivubo.

“Amini ninachokwambia, kwa kiasi tunawafahamu Enyimba” alisema. “Tunawajua ni klabu kubwa nchini Nigeria na mabingwa wa zamani wa Afrika. Tumeangalia baadhi ya video zao lakini siwezi kusema tunawajua sana Enyimba” aliongoza Nsimbe.

Nsimbe amekiri kuwaheshimu Enyimba lakini hawahofii na mipango yake ni kuhakikisha harusu bao lolote kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Inawezekana ikawa kweli Nsimbe anafahamu kiasi kuhusiana na Enyimba kwa kuwa si mgeni na wapinzani kutoka nchini Nigeria.

Mwaka 2009, KCCA chini ya George ‘Best’ Nsimbe iliifunga timu ya Bayelsa 3-1 kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Nakivubo.

Kwenye mchezio huo, mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Brian Umony aliifungia timu yake bao huku Patrick Ssenfuka akikamilisha karamu ya mabao.

Kwenye mchezo wa marudiano timu hiyo kutoka nchini Nigeria iliifunga KCCA bao 4-0 na kufanya kuwa juma ya mabao 5-3 na KCCA wakasukumizwa nje ya michuano kwenye hatua ya makundi.

Bayelsa walifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali ambapo walipoteza dhidi ya timu kutoka Algeria, ES Sentif.

Tanzania Kuanza Na Shelisheli U-17
Mabingwa Wa Soka Tanzania Bara Waahirisha Safari Ya Mauritius