Kocha George Lwandamina mejiuzulu nafasi ya ukuu wa benchi la ufundi la klabu ya Zesco United inayoshiriki ligi ya nchini Zambia.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi za klabu ya Zesco United, Lwandamina amewasilisha barua ya kujiuzulu na uongozi wa klabu hiyo kumkubalia.

”Klabu imekubaliana na kujiuzulu kwake na inamshukuru kwa kazi na mchango wake mzuri alioutoa kwa kipindi chote alichokuwa hapa.”

Lwandamina alijiunga na Zesco mwaka 2014 no kufanikiwa kushinda mataji mawili ya ligi, Ngao ya Jamii, sambamba na kuiongoza klabu hiyo kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

whatsapp-image-2016-11-07-at-15-05-38

Nafasi ya Lwandamina ambaye anahusishwa na kujiunga na klabu ya Yanga itakaimiwa na kocha msaidizi, Tenant Chembo hadi mwisho wa msimu huu.

Lwandamina hajashinda mchezo wowote wa ligi ya nchini Zambia, tangu alipoanza kuhusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na Yanga ya Tanzania.

Gerard Pique: Lionel Messi Hana Mpinzani
Gareth Southgate Kumpa Mtihani Harry Kane