Rais mteule wa Liberia, George Weah amefunga goli moja kati ya mawili ya timu yake ya ‘Weah All Stars’ katika bonanza la soka dhidi ya timu ya soka ya jeshi la nchi hiyo.

Katika bonanza hilo, Weah mwenye umri wa miaka 51 alionesha umahiri wake kama mwanasoka bora wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa), na kusababisha timu yake kushinda 2-1.

Weah akiwa mwenye furaha, ndani ya jezi namba 14 aliyoivaa pia wakati akiiwakilisha timu yake alisema kuwa anaipenda namba hiyo kwani alipewa na Taifa.

“Hii ni namba ambayo nilipewa na Taifa, kwahiyo ninaivaa… maana ya mchezo ni ushindi,” aliiambia BBC baada ya mechi hiyo ambayo ilishuhudiwa na umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa kambi ya jeshi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Bonanza hilo liliandaliwa mahususi kama utangulizi wa sherehe za kuapishwa kwa Weah kuwa rais wa taifa hilo, zitakazofanyika kesho.

Weah alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Disemba mwaka jana na anakuwa mwanasoka wa kwanza nguli barani Afrika kushika nafasi hiyo ya juu ya uongozi ndani ya taifa lake.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 22, 2018
Serikali yaitahadharisha Simba