Mchezaji wa zamani wa Soka wa Kimataifa wa Liberia, George Weah, amesema atagombea nafasi ya Urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili.

Amesema ana ndoto kubwa za kuubadilisha mfumo wa nchi hiyo.

George Weah amewahi kuzichezea klabu kubwa duniani ikiwemo PSG – Paris Saint-Germain (Ufaransa), A.C. Milan (Italia) na Chelsea Football Club (Uingereza).

Amewahi kuwa mchezaji wa Afrika wa kiwango cha juu kabisa katika orodha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ya wachezaji mashuhuri katika karne ya 20.

Alianguka katika mchakato wa mwaka 2005 baada ya kushindwa na Rais wa sasa Ellen Johnson Sirleaf, ambaye muhula wake wa pili utamalizika mwaka 2017.

Chini ya Katiba ya Liberia Sirleaf, hawezi kugombea kwa awamu nyengine.

Kipre Tchetche Kuwavaa Wekundu Wa Msimbazi Jumapili
Naibu Spika azua tafrani kwa kumuita Mbunge ‘Bwege’, Mnyika atishia Kumfikisha Mahakamani