Klabu ya Watford imetangaza kumsajili jumla Gerard Deulofeu, baada ya kumtumia kwa mkopo kuanza mwezi Januari mwaka huu akitokea FC Barcelona.

Uongozi wa klabu ya Warford inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England, umetangaza kukamilisha usajili huo wa moja kwa moja, ambao umewagharimu kiasi cha Pauni milioni 11.5, huku wakimsainisha mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka Vicarage Road hadi mwaka 2023.

Mshambuliaji huyo alikua nguzo kubwa ya kikosi cha Watford, wakati wa harakati za kupambana ili kishuke daraja msimu uliopita, na kilifanikiwa kwa kumaliza katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Deulofeu mwenye um ri wa maka 24, tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Hispania katika michezo minne, na alicheza michezo saba akiwa na Watford msimu uliopita huku akifunga bao lake la kwanza katika mchezo dhidi ya Chelsea uliochuhudia The Blues wakikubali kubamizwa mabao 4-1 mwezi Februari.

“Tuna furaha kubwa ya kumkaribisha tena  Gerard hapa Vicarage Road, na tunawashukuru FC Barcelona kwa kukubali kufanya biashara na sisi, baada ya kuonyesha tumeridhishwa na uwazo wa mchezaji huyu,” Alisema mwenyekiti wa Watford Scott Duxbury.

“Lengo letu kubwa ni kutaka kuwa na kikosi imara kitakachoweza kushindana na yoyote ligi kuu, ili tuwe sehemu ya klabu zitakazomaliza msimu katika nafasi za juu.”

Deulofeu akiwa FC Barcelona aliwahi kucheza michezo 17 msimu uliopita kabla ya kuuzwa kwa mkopo, na alifanikiwa kufunga mabao mawili, lakini alipata wakati mgumu wa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Kusajiliwa kwa Ousmane Dembele, kulimfanya mchezaji huyo kuwa na wakati mgumu zaidi katika kikosi cha Ernesto Valverde, jambo ambalo lilitoa msukumo wa kuondoka Camp Nou na kupelekwa Watford kwa mkopo mwezi Januari.

IMF yaonya kuhusu sera za Marekani
Daruso: Taarifa kuhusu marehemu kufariki na ujauzito zipuuzwe

Comments

comments