Beki wa kati wa FC Barcelona Gerard Pique, ameandika katika ukurasa wa mtandao wa Twitter, kuhusu mshambuliaji wa klabu hiyo Lionel Messi kuendelea kutangazwa kuwa mchezaji bora wa dunia tofauti na wachezaji wengine.

Pique ameandika maneno hayo huku akielekeza kijembe kwa mpinzani wa karibu wa Lionel Messi, Cristiano Ronaldo kwa kudai mshambuliaji huyo wa Real Madrid hafikii kiwango cha muagentina huyo ambaye alianza kutesa katika tuzo za ubora duniani mwaka 2009.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 29, ameibua mjadala huo, kufuatia kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na Lionel Messi kwenye mchezo wa ligi ya Hispania uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Sevilla.

Katika mchezo huo, Messi alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 43 na baadae mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Suarez alifunga bao la ushindi dakika ya 61, huku bao la kufutia machozi la Sevilla likikwamishwa nyavuni na Vitolo dakika 15 baada ya kipyenga cha kwanza kupulizwa na mwamuzi.

“Endapo tuzo ya mchezji bora duani ingekua inatolewa kwa mchezaji bora duniani kwa kuangalia kiwango, Messi alistahili kupewa kila mwaka tangu alipoanza mwaka 2009,” amesema Pique.

Katika orodha ya wachezaji ambao wanawani tuzo kwa mwaka 2016 ambayo ilitolewa mwishoni mwa mwezi uliopita na shirikisho la soka duniani (FIFA), jina la Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa waliotajwa.

Video Mpya: Rayvanny - Sugu
George Lwandamina Abwaga Manyanga Zesco United