Uongozi wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich umetoa taarifa za kuumwa kwa gwiji wa klabu hiyo Gerhard “Gerd” Müller.

Taarifa za FC Bayern Munich kuhusu gwiji huyo, zimeeleza kwamba, Gerd Müller anaugua ugonjwa uitwao Alzheimer, ambao hujikita kwenye ubongo na kuharibu kumbu kumbu.

Uongozi wa FC Bayern Munich umeahdi kuendelea kuwa sambamba na gwiji huyo, ambaye kwa sasa anaangaliwa kwa ukaribu na familia yake, huku ukiahidi kuendelea kumuenzi kutokana na mazuri aliyoifanyika klabu hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba, Müller alibainika anasumbuliwa na ugonjwa huyo mwezi februali mwaka huu, baada ya kufanyiwa vipimo, na sasa anaendelea kupatiwa matibabu.

Müller, alikuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha The Bavarians kutwaa ubingwa wa Bundesliga mara 13, kati ya mwaka 1964 na 1979.

Müller, pia aliiwezesha timu ya taifa ya Ujerumani kwa wakati huo ikiitwa Ujerumani ya Magharibu kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1974, kwa kufunga bao muhimu dhidi ya Uholanzi ambao walikubali kulala kwa mabao 2-1.

Kwa upande wa fainali za mataifa ya barani Ulaya, Müller alikuwa miongoni mwa kikosi kilichotwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka 1972.

Lukas Josef Podolski Aondoka Kambini
Kwanini Hukupata Ajira Ingawa Ulijibu Vizuri Maswali Ya Usaili..?