Rais John Magufuli ameliagiza Jeshi la Magereza liwatumie wafungwa kujenga Gereza  la Kitengule Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera lililobomoka kwa tetemeko la ardhi, Kwani  Serikali haitajenga Gereza hilo.
Katibu Mkuu Kiongozi, hakuna kuwapelekea wafungwa wa Karagwe fedha yoyote, za maafa ya tetemeko. Watetemeke na kufanya kazi,” alisema Rais Magufuli.
Alitoa agizo hilo juzi wakati akifunga mazoezi ya kijeshi ambayo kitaalamu yanaitwa ‘amphibious landing’ yaliyofanyika Kijiji cha Baatini, Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Katika mazoezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na kushuhudia wanajeshi wakilikomboa eneo lililotekwa na maadui ukanda wa majini, Rais Magufuli alimtaka Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kutopeleka fedha za maafa kujenga gereza hilo

 

Gareth Southgate Awaita 23, Glen Johnson Arejeshwa Kundini
Watafiti wa Kilimo wauawa kikatili wakidhaniwa ni wanyonya damu