Jeshi la Polisi nchini Nigeria linaendesha msako dhidi ya wafungwa zaidi ya 180 waliotoroka kutoka baada gereza kuvamiwa na watu wasiojulikana.

Idadi hiyo ya wafungwa walitoroka baada ya watu wenye silaha kuvamia gereza lililo katikati ya jiji la Minna kwenye jimbo la Niger, Jumapili usiku.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Jenerali Abdulrahman Dabazzau amesema kuwa wafungwa 30 waliojaribu kutoroka walikamatwa lakini 189 hawajulikani walipo. Aidha, maafisa wa jeshi hilo wamedai kuwa huenda idadi ya waliotoroka ikawa ni zaidi ya iliyotajwa awali.

“Kati ya 219 waliokuwa wametoroka, tulifanikiwa kuwakamata tena 30,” alisema Rabiu Shuaib, msemaji wa Jeshi la Magereza, hali inayoonesha kuwa wafungwa 189 hawajulikani walipo.

Uvamizi wa magereza hufanyika nchini Nigeria na hutekelezwa na kundi la kigaidi la Boko Haram pamoja na makundi mengine ya kihalifu.

Mamlaka ya Magereza nchini humo imeeleza kuwa upelelezi unaendelea kufanyika kuhusu tukio hilo ili kubaini waliotekeleza uvamizi huo na kuwakamata.

Arsenal yampigia hesabu Marouane Fellaini
Jafo awataka waamuzi UMISSETA na UMITASHUMTA kuzingatia kanuni