Katika jitihada za serikali kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora bado suala hili limezidi kuwa na changamoto tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na wimbi kubwa la wanafunzi waliojiunga na shule hali inayosababisha shule nyingi kuwa na upungufu wa madawati.

Baada ya kuchangia harambee za kuusaidia mkoa wa Geita kuweza kupata madawati Mdau wa maendeleo ya Elimu Mkoani hapo Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu Geita (GGM)  Terry Mulpeter, jana amekabidhi madawati elfu kumi yenye thamani ya shilingi milion 750 yagawanywe katika wilaya tano zilizopo ndani ya mkoa huo.

Akipokea msaada huo kutoka GGM kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya  Herman Kapufi amesema Geita wanaithamini na kuitambua michango yote ya kimaendeleo inayofanywa na GGM  pia kuahidi wanafunzi kufanya vizuri kwani ufaulu wa wanafunzi unazidi kuimarika na kuridhisha huku akiwataka wadau wengine wajitokeze kuchangia maendeleo ya elimu Mkoani hapo

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya madawati Mulpeter amesema kwamba tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa huo limewagusa GGM kama majitani na wadau wakubwa wa maendeleo ya elimu lakini pia kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha elimu.

Aidha Mulpeter alisema kuwa Kampuni yake itazidi kuchangia maendeleo ya elimu na kwamba elimu ndio msingi wa mabadiliko na maendeleo katika jamii yoyote duniani.

Mpaka sasa mgodi huo umekwisha tumia bilioni 10 za kitanzania katika kusaidia maendeleo ya elimu katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na kujenga shule ya sekondari ya bweni ya wasichana itakayosaidia zaidi ya wasichana 800, Ujenzi wa Maabara na Maktaba ya kisasa na kushiriki katika ujenzi wa madarasa maeneo mbalimbali Mkoani Geita

Wanafunzi shule binafsi kunyimwa mikopo
Video: ACT Wazalendo wapinga utaratibu utoaji mikopo elimu ya juu