Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GMM), Manase Ndoloma, amesema kuwa wimbi la idadi ya watoto wadogo wanaovamia mgodi huo usiku kuiba mchanga wenye dhahabu linaendelea kuongezeka kila mwaka.

Ndoloma amesema kuwa tangu mwaka huu uanze Watoto 941 wamekamatwa, wakati mwaka uliopita walikamatwa watoto 815 wanaovamia mgodi huo usiku kuiba mchanga wa dhahabu.

Ameyasema hayo alipokutana na wadau mbalimbali mkoani Geita kujadili changamoto ya kuongezeka kwa watoto na watu wazima wanaovamia mgodi kuiba mchanga wa dhahabu katika eneo la uchimabaji na kutafuta mbinu za kulitatua tatizo hilo.

“Nakumbuka mwaka 2012 tulimkamata mtoto mmoja ambaye umri wake hauzidi miaka 10, Tulimhudumia vizuri kwa kumpa chakula na mavazi na kumhoji kiurafiki na baadaye kumrudisha nyumbani,” amesema Ndoloma.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ukarimu huo ulikuwa kama kosa kwasababu baada ya hapo wimbi la watoto wavamizi liliongezeka.

Ndoloma amewaomba wazazi kuacha kuwatumia watoto kutekeleza uvamizi kwenye mgodi huo, ambapo hadi sasa watu 790 wamesha funguliwa mashtaka kwa uvamizi wa mgodi.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 10, 2018
Taifa Stars yaendelea kujifua Afrika kusini, Kakolanya, Zayed wakosa mazoezi

Comments

comments