Wafanyakazi wa kike wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited – GGML ladies, wametoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali kwa akina mama Wajawazito na Wazazi katika hospitali ya Nzela na kituo cha Afya Kasota zilizopo Halmashauri ya Wilaya Geita.

Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo, Makamu mwenyekiti wa kikundi hicho, Lina Sitta amesema wanawake wanaofanya kazi GGML wameguswa na changamoto za uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya katika vijiji vinavyowazunguka.

Mmoja wa wafanyakazi wanawake wa GGML kutoka idara ya uchakataji dhahabu, Rehema Lusendamila akimjulia hali mgonjwa aliyelazwa katika Kituo cha Afya Kasota. Katikati ni Lina Sitta – Makamu mwenyekiti wa kikundi cha wafanyakazi wa kike wanaofanya kazi katika kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML ladies).

Amesema, “Tumeona tuanze na vijiji vya Kasota na Nzela vilivyopo karibu na mgodi wa GGML tumeona akina mama wakikosa sabuni, taulo za mama waliojifungua na nepi za watoto. Msaada huu ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.”

Naye Mganga Msaidizi wa kituo cha afya Kasota, Stanley Victor amewashukuru Wanawake hao kwa kutoa msaada na GGML kusaidia ujenzi wa maabara, nyumba ya mtumishi na jengo la baba na mtoto kituoni hapo.

GGML Ladies – Geita.

Amesema, “Mmeitendea haki siku ya wanawake duniani mwaka huu.Wagonjwa wengi waliopo hapa wamefarijika sana kutokana na msaada huu,” huku kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ikiwa ni Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia: chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.

Jukwaa la Maendeleo ya Utamaduni lajipanga kukuza Utamaduni
Ahmed Ally: Tumemaliza shangwe za ushindi