Timu za taifa za kutoka Afrika zitaendelea kukutana katika fainali za kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zinazoendelea mjini Mumbai nchini India.

Ghana watapambana na Mali, baada ya kumalizana na Niger katika mchezo wa hatua ya 16 bora kwa kuchapa mabao mawili kwa sifuri, mchezo uliochezwa leo mchana kwa saa za Afrika mashariki.

ric Ayiah alianza kuifungia Ghana bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati, na baadae Khaled Lawali mlinda wa Niger, alifanikiwa kupangua penati nyingine ya Ghana iliyopigwa na mchezaji huyo katika dakika ya 86.

Hata hivyo kazi hiyo ilikua sawa na bure kutokana na kikosi cha Niger kushindwa kusawazisha hadi dakika ya 90, ambapo Ghana walifanikiwa kupata bao la pili na la ushindi kupitia kwa Richard Danso dakika za lala salama.

Kocha mkuu wa Ghana Samuel Fabin, amesema dhamira yake kubwa baada ya ushindi wa hii leo, ni kutaka kuiwezesha nchi yake kufikia mafanikio ya mwaka 1991 na 1995, ambapo walitwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Hali kadhalika upande wa Mali ambao walimaliza katika nafasi ya pili kwenye fainali za 2015, watakua na dhamira ya kutotaka kutolewa mapema katika michuano ya mwaka huu, ili kufika hatua ya fainali na kurekebisha makosa yao.

Mchezo mwingine wa hatua ya 16 utakaochezwa baaye hii leo, utakua kati ya kikosi cha Brazil dhidi ya Honduras.

Jose Mourinho aikana kauli yake
Aliou Cisse apingana na ripoti ya Liverpool, amuita Mane