Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema kwa sasa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ina uwezo wa kuhudumia watoto 250 hadi 300 kwa mwaka, ambayoni sawa na asilimia kumi ya mahitaji yote na kwamba gharama za upasuaji kwa mtoto mmojani ghali na huanzia Sh. milioni 2 hadi Sh. milioni 11 kwa kutegemea na ukubwa wa tatizo.

Dkt. Mpango ameyasema hayo hii leo Agosti 14, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na washiriki wa tamasha la marathon lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kuhudhuriwa na wananchi, Viongozi, Wanadu mbalimbali wakimemo DataVision International Jogging.

Amesema, “Kwahiyo mtakubaliana nami kwamba gharama hizi ni kubwa kwa Mtanzania wa kawaida na kwa takwimu zilizopo mpaka kufikia mwezi juni 2022, Hospitali hiyo imekuwa na wagonjwa takriban 750 ambao walihitaji kufanyiwa upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo.”

Dkt. Mpango ameongeza kuwa, hali hiyo inaonesha namna tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa nchini na kudai kuwa fedha wanazochangia zitasaidia kufanikisha kuokoa maisha ya wagonjwa wengi ambao walikuwa wameshakata tamaa ya kupata matibabu.

Aidha, Makamu wa Rais amesema pia amefurahishwa na mpango wa Benki ya CRDB kwa kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia akina mama wenye ujauzito hatarishi ili waweze kupata huduma na kuokoa uwezekano wa kumpoteza mtoto, mama au wote kwa pamoja.

“Japokuwa kwasasa hakuna takwimu maalum za kuonesha idadi y akina mama wenye ujauzito hatarishi, lakini sisi wote ni mashahidi kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na uhitaji mkubwa wa huduma ya dharula kwa akina mama wajawazito wakati wa kujifungua,” amefafanua Dkt. Mpango.

Kenya: Mgombea Urais akubali kushindwa
Kenya: IEBC yasema mfumo wa kuhesabu kura haujadukuliwa