Wakala wa mchezaji bora wa dunia kwa mara nne Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes ameweka hadharani kiasi ambacho timu za ligi ya China inapaswa kukitoa ili mchezaji wake huyo acheze ligi hiyo.

Mendes ameiambia Sky Sports Italia, kama kuna timu ya China inamtaka Ronaldo inapaswa kutoa kiasi cha paundi milioni 260 kwa Real Madrid na mshahara wa paundi milioni 1.6 kwa wiki kwa ajili ya mchezaji wake.

Kiasi hicho cha fedha ya uhamisho wa mchezaji huyo kitakuwa ni zaidi ya mara tatu ya dau alilonunuliwa na Madrid mwaka 2009 akitokea Manchester United ambapo alinunuliwa kwa paundi milioni 80.

”Kutokana na ubora wa kidunia wa mchezaji huyo, hivyo sio rahisi kwa ligi za China kumnunua mchezaji huyo” Alizungumza Mendes

 

Zitto Kabwe atoa tamko kuhusiana na mshahara, madeni na mali anazomiliki
Uhuru amtumia salamu za heri ya Krismasi mbunge aliyemtukana hadharani