Takriban watu 174 wamefariki, na wengine zaidi ya 180 kujeruhiwa katika uwanja wa mpira wa miguu nchini Indonesia, baada ya maelfu ya mashabiki wa waliokuwa na hasira kuvamia uwanja na Polisi kuwarushia mabomu ya machozi hali ambayo ilisababisha kuanguka na kukanyagana.

Tukio hilo, limetokea usiku wa Jumamosi Octoba 1, 2022 katika mji wa Malang, nchini Indonesia kufuatia mashabiki hao kupandwa na hasira baada ya timu yao ya Arema FC kufungwa 3-2 na timu pinzani ya Persebaya Surabaya kwenye uwanja wa Kanjuruhan.

Uharibifu baada ya tukio la watu kufariki uwanjani nchini Indonesia. Picha na shine.cn

Polisi nchini humo, ambao walilitaja tukio hilo kama machafuko, walijaribu kuwashawishi mashabiki kurudi kwenye maeneo yao ya kuketi lakini haikuwezekana na hivyo kutumia vitoa machozi baada ya wenzao wawili ambao ni maafisa Polisi kuuawa na magari yao kuharibiwa.

Ingawa idadi ya wanahabari inasema watu 174 wamefariki, lakini Mkuu wa Polisi wa Java Mashariki, Nico Afinta kupitia taarifa yake ya hii leo Octoba 2, 2022 amesema kuna vifo 127 na kuanisha kuwa wawili kati yao ni maafisa wa Polisi, 34 walikufa ndani ya uwanja na waliosalia walifia hospitalini.

Sehemu ya matukio yaliyosababisha mauaji baada ya matokeo ya mpira. Picha na The news chronicle.

Katika tukio hilo, baadhi ya watu walijitolea kuwabeba majeruhi, na hii leo asbuhi (Jumapili, Octoba 2, 2022)imeshuhudiwa Magari kadhaa yaliyochomwa moto, likiwemo lori la polisi, na mengine yalitapakaa mitaani na nje ya uwanja kutokana na vurugu hizo.

Hata hivyi, tayari Serikali ya Indonesia imeomba radhi kwa tukio hilo na Waziri wa Michezo na Vijana wa Indonesia Zainudin Amali, ameahidi kuchunguza mazingira ya mkanyagano huo na kusema “Tunasikitika kwa tukio hilo la kusikitisha, limeleta majeraha kwenye soka la nchi yetu.

Mabadiliko baraza la Mawaziri
Bil. 2.7 zatolewa 'kupiga jeki' utafiti Tiba Asili