Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia Giampiero Ventura amemjibu mshambuliaji wa klabu ya Nice ya  nchini Ufaransa Super Mario Barwuah Balotelli.

Ventura amejibu Balotelli kwa kuzungumzia uwezekano wa kumuita katika kikosi chake katika mchezo ujao wa kimataifa wa timu ya taifa ya Italia, ambayo ipo kwenye mchakato wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Kocha huyo amesema anafuatilia michezo ya Ufaransa hususan michezo inayoihusu klabu ya Nice, na ameanza kuridhishwa na uwezo wa mshambuliaji huyo.

Amesema mshambuliaji huyo ameonyesha mabadiliko makubwa, na anaamini uzoefu wa kucheza michuano mikubwa kama kombe la dunia, unamsaidia kufanya vyema katika ligi ya nchini Ufaransa.

“Amecheza fainali za kombe la dunia, hivyo ninatarajia kumtumia katika michezo itakayotukabili siku za usoni,” Alisema Ventura.

“Kwa sasa tuna muda wa kutosha hadi mwezi Machi, ambapo kutakua na michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia, nitaendelea kumfuatilia ili niendelee kuthibitisha uwezo wake kikamilifu.”

Majibu wa Ventura, yanakuja baada ya juma moja kupita ambapo Boletelli alizungumzia matamanio ya kuitumikia timu ya taifa lake, ambayo hajaichezea kwa muda mrefu.

Hata hivyo Balotelli aliahidi kucheza kwa kujituma akiwa na klabu yake ya Nice, ili kumridhisha kocha Ventura, na dhahir ombi lake limeanza kupata majibu ya kuridhisha.

Steven Gerrard Ajihukumu
Ommy Dimpoz ajibu tuhuma za ‘ushoga’ alizotupiwa na Diamond