Aliyekua mshambuliaji wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Juventus FC Gianluca Vialli, amesema naendelea vyema kiafya, baada ya kujiuguza maradhi ya saratani kwa kipunidi cha mwaka mzima.

Gwiji huyo mwenye umri wa miaka 54, amethibitisha utimamu wake wa mwili alipozungumza na mwandishi wa gazeti la Corriere Della Sera la Italia, na kusema anamshukuru mungu anaendelea vyema baada ya matibabu.

“Nipo vizuri, ninaendelea vyema kiafya. Imenichukua mwaka mzima kujiuguza maradhi haya ya saratani, leo ninamshukuru mungu hadi unavyoniona.” Alisema Vialli.

“Lakini nikuhakikishie kwamba nitaendelea kuwa sehemu ya jamii kama kawaida, japo hatujui lililopangwa kesho kuhusu maisha yangu. Ninatumai nitaendelea kuwa salama.”

Vialli alijenga jina lake kimamilifu alipokua na klabu ya Sampdoria kuanzia mwaka 1984–1992, na baadae alijiunga na mabingwa wa soka nchini Italia kwa sasa Juventus FC na alifanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 1996.

Baadae alielekea nchini England kujiunga na klabu ya Chelsea, ambayo aliifungia mabao 48 katika michezo 78 aliyocheza, kabla ya kutangazwa kuwa meneja wa klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Luis Suarez kusubiri hadi Disemba
TCRA yataja wamiliki wa Wasafi TV, Kusaga hakutajwa