Mlinda mlango mkongwe wa Italia Gianluigi Buffon, amepongeza hatua ya mshambuliaji Mario Balotelli ya kujiunga na klabu ya OGC Nice ya Ufaransa.

Buffon amesema hatua hiyo ni kubwa kwa Balotelli ambaye ilionekana huenda kipaji chake kingepotea, endapo angeshindwa kupata mahala pa kucheza soka lake kabla ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa kuamkia jana.

Mlinda mlango huyo ambaye pia anaitumikia klabu bingwa nchini Italia Juventus FC, amesema Balotelli amekua na kipaji kizuri cha kucheza soka lakini changamoto kadhaa zinazomkabili mara kwa mara, zimekua zikiwakatisha tamaa watu wake wa karibu.

“Nimefarijika kusikia amepata mahala pa kucheza, binafsi ninampenda sana Belotelli amekua na kiwango cha tofauti anapokua uwanjani, wakati mwingine huwa natamani nichezenaye katika klabu moja,”

“Kwangu mimi sijali amepata wapi nafasi ya kucheza soka lake, lakini kikubwa kilichonifurahisha ni Balotelli kuendelea kuwa sehemu ya wachezaji ambao kwa msimu huu watacheza soka, na nina matarajio makubwa ya kumuona akirejea katika kiwango chake.” Alisema Buffon

Balotelli alipewa ruhusa na kusaka klabu ya kuitumikia kwa msimu wa 2016/17, baada ya meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kumuengua katika mipango yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alikua na wakati mgumu wa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Liverpool tangu aliposajiliwa miaka miwili iliyopita chini ya utawala wa Brendan Rodgers, hali ambayo ilipelekea atolewe kwa mkopo kwenye klabu ya AC Milan.

Jina La Bastian Schweinsteiger Lapitishwa Old Trafford
Man City Kumpigania Sergio Aguero