Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino ameonyesha kuchukizwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi, vinavyoendelea katika ligi ya Italia na pahala pengine ulimwenguni.

Infantino amedhihirisha kuchukizwa na hali hiyo, kufuatia sataka lililojitokeza jana jumapili wakati wa mchezo wa ligi ya Italia (Serie A) kati ya Atalanta dhidi ya Fiorentina, uliomalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Katika mchezo huo, mshambuliaji wa pembeni kutoka Brazil na klabu ya Forentina Dalbert Henrique, alimlalamikia mwamuzi Daniele Orsato, kufuatia vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyokua vikionyeshwa na mashabiki wa timu ya Atlanta kwenye uwanja wa Ennio Tardini mjini Parma.

Mashabiki wa Atlanta walisikika wakitoa milio ya Sokwemtu, wakati wote mchezaji huyo alipomiliki mpira mguuni mwake.

Mwamuzi aliafiki ombi hilo, na mashabiki walitangaziwa kuacha vitendo vya kibaguzi dhidi ya mchezaji huyo.

“Vitendo vya kibaguzi vinaendelea kushamiri siku hadi siku, ninashangazwa na hali hii, kwa sababu mchezo wa soka mara nyingi unatumika kama sehemu ya kukataza baadhi ya mambo machafu katika jamii, lakini kwa nini tunashindwa kuliondoa hili la ubaguzi? ” alihoji kiongozi huyo wa juu wa FIFA, alipokua mgeni rasmi katika moja ya vipindi vya televisheni ya Rai ya Italia.

“Vitendo hivi havitavumilika tena, tutaendelea kupambana navyo, hadi wahusika waelewe nini tunachomaanisha. “Hakuna haja ya kuendelea kufanya vitendo hivyo vya kinyama dhidi ya wanaadamu wengine, hakuna alie mbora dhidi ya mwingine, sisi sote tupo sawa.”

Juma lililopita klabu ya Cagliari almanusura iadhibiwe na chama cha soka nchini Italia, kutokana na vitendo vya ubaguzi wa rangi alivyofanyiwa mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku.

Katika mchezo huo mashabiki waliodhaniwa kuwa wa Cagliari walisikika wakilia kama Sokwemtu, pindi mshambuliaji huyo kutoka nchini Ublegiji alipomiliki mpira kuelekea kangoni mwa wapinznai wake.

Washtakiwa 5 kesi ya uhujumu uchumi waachiwa huru
Rais Magufuli atoa siku 7 wahujumu uchumi kutubu