Hongera zimfikia msanii wa muziki wa bongo fleva nchini aliyefanya vizuri na kibao chake cha Papa, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, kwani amefanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike na kumpatia jina la Myra.

Gigy Money anatoka kimapenzi na mtangazaji wa Choice FM, Moj360 ambaye pia ni baba mzazi wa mtoto huyo aliyezaliwa siku ya leo.

Gigy na Moj360 kabla ya kuzaliwa kwa mtoto huyo walikuwa wakijiita Baba Candy na Mama Candy ila mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo wamesema hawatatumia tena jina hilo na tayari wamempa mtoto wao jina la Myra.

Gigy Money amekuwa msiri sana katika swala hili la mimba kwani pamoja na umaarufu wake, mashabiki wake waligundua juu ya mimba hiyo ikiwa na miezi saba na akiwa amebakiza miezi  miwili kujifungua.

Hata hivyo sakata la BASATA ndio lililofanya mashabiki na kipenzi cha msanii huyo kujua juu ya mimba hiyo mara baada ya TCRA Kumfungia nyimbo yake ya Papa na kumtaka kujisajili Baraza la Sanaa Tanzania.

Gigy ni moja kati ya wasanii wachache waliopata umaarufu wao kupitia mtandao wa kijamii wa instagram kwa kuposti picha za nusu uchi, baada ya kupata umaarufu huo Gigy Money aliamua kujikita na sanaa ya muziki, mbali na muziki kwa sasa Gigy Money ni mtangazaji wa kipindi cha Choice Fm.

 

Iniesta amwaga chozi wakati akiaga Barcelona
Unai Emery kufungasha virago Parc des Princes

Comments

comments