Msanii  wa bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money anayetamba na wimbo wake wa chanyanga,  ameseama kuwa hivi karibuni kwenye siku yake ya kuzaliwa atavalishwa pete ya uchumba na mchumba wake mpya ambae pia ni mwanamziki mwenzake kutoka Nigeria.

Amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Refresh na Wasafi Tv wakati akieleza mipango yake ya mbeleni na mchumba wake ambaye anaishi naye kwa sasa na tayari wamesha shirikiana kwenye kazi ya muziki

Ameongeza kuwa mbali na mapenzi kwa sasa anaangalia sana kufanya kazi ambapo anajiandaa kutoa albamu ya nyimbo zake.

Aidha amesema wanenguaji (video vixin) wengi wamekuwa wanaingia kwenye muziki kutokana na ushawishi wanaoupata kutokana na wasanii wanaofanya nao kazi, ameongeza mbali na kazi yeye ni mama na anafanya muziki kwa malengo.

 

Watatu mbaroni kwa kukutwa na kobe 508
Al - Bashir kuhojiwa kwa utakatishaji wa Fedha

Comments

comments