Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Olivier Giroud amesema ana shauku ya kucheza sambamba na Mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic katika kikosi cha AC Milan ya Italia.

Giroud ametoa kauli hiyo, huku Mashabiki wengi duanini wakiamini kucheza pamoja kwa wawili hao kutaleta manufaa makubwa kwenye kikosi cha AC Milan, kilichodhamiria kutwaa ubingwa wa Italia msimu huu 2021/22.

Amesema Ibrahimovic ni kama alama ya hamasa kwa wachezaji vijana kwenye Ligi Kuu ya Italia, Serie A, huku akielezea namna anavyosubiri kwa hamu kucheza na mshambuliaji huyo wa Sweden pale AC Milan.

Kwa mabao yake hayo mawili, raia huyo wa Ufaransa alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mara mbili kwenye mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa ‘Rossoneri’ hao tangu Mario Balotelli aliyefanya hivyo, Februari 2013.

Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, mwezi uliofuata alikutwa na maambuzi ya COVID-19 na hivyo kulazimika kujitenga na kukosa kucheza na kuwaacha, Rafael Leao na Ante Rebic wakiongoza mashambulizi kwa kikosi hicho cha kocha, Stefano Pioli.

Ibrahimovic amefunga mara moja licha ya kucheza dakika 30 tu kwa miamba hao wa Serie A msimu huu, na amekuwa nje kutokana na majeraha.

Na sasa Giroud ana hamu kubwa ya kucheza pamoja na mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona na Manchester United.

“Nilicheza dhidi ya Zlatan mara chache,” amesema Giroud kupitia YouTube channel.

“Yeye bado anacheza katika umri wa miaka 40 na hi maana yake ni mchezaji wa aina yake.”

“Anajitunza mwenyewe na mwili wake, na mimi pia nitajaribu kufanya hivyo kadri mwili wangu utakavyoniruhusu.”

Olivier Giroud alisajiliwa na AC Milan Julai 17 2021, akitokea Chelsea ya England kwa mnkataba wa miaka miwili, huku ada ya uhamisho wake ikifanywa siri.

Volkano ya Tope Kunduchi hatari
Southgate kusaini mkataba mpya England