Kiongozi wa East Coast Team, King Crazy GK amedai kuwa angepewa nafasi angeutumia uhasama uliopo kati ya Ali Kiba na Diamond kuwafanya kuwa mabilionea.

diamond-na-ali-kiba

GK ambaye mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiiongoza East Coast Team aliupika uhasama mkubwa kati ya kundi hilo na TMK Wanaume wakiongozwa na Juma Nature, amesema kuwa angechochea kuni ugomvi wa mastaa hao ili unoge na baadae uzae tamasha kubwa kuwahi kutokea nchini.

“Kwanza nitaongeza conflict, ule mgongano sitoupunguza, nitauongeza, nitazidi kuuvibrate uwe mkubwa watu wa waufeel. Sasa upo upinzani kwa Kiba na Diamond zaidi personal, sasa mimi nitauweka watu wauvae yaani wakikutana pale inakuwa noma,” alisema GK.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo angetengeneza ajenda kuhusu wawili hao na kufanya mpango kabambe ambao mwisho wa siku wangeweza kusimama wakapiga show kubwa katika uwanja wa Taifa.

Gwaimaka anapowaza pesa mwacheni aitwe King Crazy GK!

Video: Magufuli aiunganisha familia ya Dk Masaburi
Mungai ajivua lawama, Adai elimu ilianza kuporomoka enzi za Kikwete