Rapa Mkongwe ambaye mwanzoni mwa miaka ya 2002 alitajwa kuwa mmoja kati ya rappers bora zaidi nchini, ameamua kuachana na muziki huo na badala yake amegeukia uimbaji.

GK amesema kuwa hivi karibuni anajipanga kuachia wimbo wake wa kuimba na kwamba amefanya mabadiliko hayo kutokana na kuwepo ushindani mkubwa hivi sasa hata kutoka kwa wasanii wa nje ya nchi.

“Nimeamua kuimba lakini ni kutokana na game la Tanzania kubadilika, zamani tulikuwa tukishindana sisi wa Tanzania kama Juma Nature, AY na wengine lakini kwa sasa muziki wa Bongo ume’change’ na kuingia mpaka wakina Wizkind, so kubadilika muhimu” GK ameiambia ENews ya East Africa TV.

Rapa huyo ambaye alikuwa kiongozi wa ngome ya ‘East Coast Team’, iliyokuwa na wasanii kama AY, Mwana FA, O-Ten, Snare na wengine, amesema kuwa hivi sasa amejipanga kufanya mashambulizi makali zaidi ili aendane na game.

 

Ukongwe Na Uwajibikaji Vyampa Heshima Wayne Mark Rooney
Lipumba amvaa Maalim Seif,adai ana ‘Udikteta’, amkana Mtatiro