Msanii wa muda mrefu katika muziki wa Hip Pop nchini, Gwamaka kaiula anayejulikana kwa jina la ‘King Crazy GK’ ametaka wasanii warudi shule ili waondokane na utumwa.

Crazy GK alifunguka kuwa wasanii wengi wamekuwa wakipelekeshwa na watu kwa madai kutokana na elimu ndogo waliyo nayo wengi wao, huku akidai kuwa kama wangekuwa na elimu wangefanya kazi yao kwa ufasaha.

Kuna baadhi ya wasanii wanajutia nafasi waliopoteza kwenye suala zima la elimu, namchukulia Mr. Blue kama mfano wa msanii aliokataa shule lakini sasa anatamani angesoma. Wasanii inawapasa kutambua muziki una umri, kuna miaka ukifikia huwezi fanya muziki lakini ukiwa na elimu  inauwezo wa kukupeleka kokote duniani na kujiamini kukabiliana na changamoto mbalimbali.

”Wasani warudi shule, wengi wamekuwa wakipelekeshwa kwa kuwa hawana elimu, kama mtu ukiwa na elimu yako unaweza ukajiamlia mwenyewe cha kufanya kutokana na elimu uliyokuwa nayo na kikawa kitu kizuri zaidi ,” amesema Crazy GK.

GK kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya ”Mzuri Pesa” ameongeza kwa kusema ngoma zake nyingi amekuwa akiwatumia waongozaji (director) kutoka nje kwani wao hujua wasanii wanataka nini.

Marseille Yavunja Mkataba Na Lassana Diarra
Hull City Kujibu Tuhuma Mbele Ya FA