Shirikisho la soka kusini mwa Amerika (CONMEBOL) limethibitisha kutumia tekenologia ya utambuzi wa mpira kuvuka mstari wa goli (Goal Line Technology) wakati wa fainali za mataifa ya ukanda huo ambao zitaanza kuunguruma mwanzoni mwa mwezi ujao nchini Marekani.

Maamuzi ya kutumika kwa mfumo huo, yamepewa baraka katika mkutano mkuu wa CONMEBOL, uluiofanyika jana nchini Marekani kwa kuishirikisha kamati ya waamuzi ya shirikisho hilo.

Kusudio kubwa la kuanza kutumiwa kwa mfumo huo kwenye michuano ya Copa America, ni kutaka kumaliza mzozo ambao umekua ukijitokeza mara kwa mara katika medani ya soka kuhusu maamuzi ya kukubalika ama kukataliwa kwa bao lenye utata.

Mkutano huo mkuu wa CONMEBOL, pia ulitangaza orodha ya waamuzi 18 watakaochezesha fainali hizo ambazo zitakua zitasherehesha miaka 100 ya kuanzishwa kwa shirikisho hilo.

Mark Geiger

Miongoni mwa waamuzi hao 18, watatu wanatokeo nchini Marekani ambao ni Mark Geiger, Jair Marrufo pamoja na Armando Villarreal.

Geiger amewahi kuchezesha michezo mitatu ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zilifanyika nchini Brazil, ikijumuisha mpambano wa hatua ya mtoano ambao ulishuhudia Ufaransa wakipambana na timu ya taifa ya Nigeria.

Mchezo huo ulimpandishia hadhi Geiger na kumfanya awe muamuzi wa kwanza kutoka nchini Marekani kuchezesha mpambano wa fainali za kombe la dunia hatua ya mtoano.

Waamuzi wengine waliotajwa kwa ajili ya kupuliza filimbi katika fainali za Copa America za mwaka 2016 ni Joel Aguilar (El Salvador), Jose Argote (Venezuela), Julio Bascunan (Chile), Enrique Caceres (Paraguay), Victor Carrillo (Peru), Andres Cunha (Uruguay), Roberto Garcia (Mexico), Heber Lopes (Brazil), Patricio Loustau (Argentina), Yadel Martinez (Cuba), Ricardo Montero (Costa Rica), John Pitti (Panama), Wilmer Rodan (Colombia), Gery Vargas (Bolivia) and Roddy Zambrano (Ecuador).

Leicester City Waanza Kuuza Wachezaji Wao
Silvio Berlusconi: Hatujaridhishwa Na Balotelli

Comments

comments