Rapa Godzilla amemchana kwa mara nyingine mwanafamilia wa Tamaduni Music, Nikki Mbishi akidai kuwa ni mchenguaji asiyekuwa na wimbo mkali (wack rapper).

Zilla amemrushia makombora rapa huyo alipokuwa akifanya mahojiano hivi karibuni na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, ambapo alitakiwa kueleza nani mkali wa mitindo huru kati yao.

“Nikki Mbishi is just a wack rapper, hana hit song, Nikki mbishi is struggling (Nikki Mbishi anahangaika). Lakini kitu kimoja naweza kumshape nikampatia hit song. halafu sio sehemu nyingine yoyote, nitampigia beat mimi in my own production.  I’m gonna make him famous again (nitamfanya kuwa maarufu tena),” alisema Zilla.

Aliongeza kuwa wimbo wa mwisho mkali wa Nikki Mbishi alifanya naye, ulikuwa unaitwa ‘Kila Siku’ na baadae akatoa ‘Play Boy’. Lakini sasa anataka kumrudisha kwenye umaarufu.

Wasanii hawa waliwahi kuwa na ushindani mkubwa katika mitindo huru miaka kadhaa iliyopita kabla ya kushirikiana kufanya ngoma kadhaa baadae. Moja kati ya nyimbo zao zilizozua mjadala wa nani amemfunika mwenzie ni ‘Kill Yourself’, ngoma ya Nikki Mbishi aliowapa shavu Mfalme wa Salasala na Cliff Mitindo.

Kimenuka! Mayweather na McGregor, waweka wazi tarehe ya pambano
Uli Stielike Atupiwa Virago

Comments

comments