Timu ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors imefanikiwa kujiandikishia ushindi katika mchezo wa kwanza wa fainali ya NBA dhidi ya Cleveland Cavaliers kwa kuifunga vikapu 104 – 89 huko Oakland allfajiri ya leo Julai 3.

Kutokana na matokeo hayo, sasa Golden State Warriors  wanaongoza kwa 1 – 0 katika michezo saba bora (best of seven ambayo itachezwa).

Ili mshindi apatikane ni lazima apate ushindi wa michezo minne dhidi ya mpinzani wake.

Michezo mingine ya fainali kati ya Golden State Warriors dhidi ya Cleveland Cavaliers imepangwa kuchezwa Juni 5, Juni 8, na Juni 10. Stephen Curry

Enddapo Golden State Warriors itapata ushindi katika michezo mitatu ijayo mfululizo itatangazwa kuwa bingwa lakini kama Cleveland Cavaliers watapata ushindi katika moja ya michezo hiyo michezo mingine itaongezwa.

hii ni fainali ya pili mfululizo kwa timu hizi kukutana. Katika fainali ya mwaka jana Golden State Warriors ilipata ushindi wa 4 – 2 shidi ya Cleveland Cavaliers.

ACT Wazalendo Kumpokea Zitto Kabwe Kimkakati, baada ya kulimwa adhabu Bungeni
Video Mpya: Rich Mavoko - Ibaki Story