Timu ya Golden State Warriors imevunja rekodi ya NBA ya kufikisha idadi ya michezo mingine zaidi waliyopata ushindi kwa msimu moja baada ya kuilaza Memphis Grizzlies point 125 – 104 na kumaliza msimu ikiwa  imejikusanyia ushindi mara 73 na kushindwa mara 9.

Ushindi huo uliopatikana usiku wa kuamkia hii leo umevunja rikodi iliyowekwa na timu ya Chicago Bulls msimu wa mwaka 1995-96, ikiongozwa na gwiji Michael Jordan.

Stephen Curry

Nyota wa Warriors Stephen Curry, pia alivunja rikodi nyingine binafsi na kua mchezaji wa kwanza katika historia ya mpira wa vikapu kupachika pointi 400 kutokana na kutumbukiza wavuni mpira kutoka eneo la pointi tatu.

Mwakyembe: Bora watanzania Tufe…
Kobe Bryant "The Black Mamba" Astaafu Kwa Heshima